Unyanayasaji wa Kutumia Picha

Je, Unyanayasaji wa Kutumia Picha ni Nini?

Unyanyasaji wa kutumia picha hutokea mtu anaposhirikisha au kutishia kushirikisha picha au video za faragha za kwako bila ruhusa yako. Aina hii ya unyanyasaji mara kwa mara ni sehemu ya ukatili wa nyumbani, familia, na kingono.

Nchini Australia, kushirikisha picha za ngono bila idhini au kutumia picha kusaliti mtu ni kinyume na sheria. Unaweza kuripoti vitendo hivyo kwa polisi na eSafety Commissioner.

Unyanyasaji wa kutumia picha ni tatizo kubwa kwa sababu huvamia faragha yako nauinaweza kusababisha madhara makubwa. Kuelewa aina hii ya unyanyasaji ni muhimu ili kujilinda mwenyewe na wengine. Kwa kujua haki zako na kutafuta usaidizi, unaweza kupata udhibiti tena na kuhakikisha usalama wako.

Chini ya sheria ya Australia

  • Una haki ya ufaragha na usalama.
  • Unyanyasaji wa kutumia sanamu kamwe siyo kosa lako.
  • Msaada unapatikana, na hauko peke yako.

Aina za Unyanayasaji wa Kutumia Picha

Unyanyasaji wa kutumia picha unaweza kutokea katika aina nyingi. Hapa chini ni baadhi ya mifano:

  • Kushirikisha Picha za Kibinafsi Bila Idhini: Kuweka au kutuma picha au video za kibinafsi za kwako bila ruhusa yako.
  • Kutishia Kushirikisha Sanamu: Kutumia kitisho cha kushirikisha sanamu za kibinafsi ili kukudhibiti au kukuhofia.
  • Kuaibisha kwa kutumia Tamaduni au Dini: Kushirikisha picha zinazoonyesha vibaya desturi zako za kitamaduni au za kidini bila ruhusa yako.
  • Kuhariri Sanamu: Kubadilisha picha ili kukuonyesha vibaya na kisha kuzishirikisha.
  • Kutumia Sanamu kwa Usaliti: Kudai pesa au upendeleo badala ya kutoshirikisha picha.
  • Kusambaza Sanamu Kwa Upana: Kushirikisha picha za kibinafsi kwenye mitandao ya kijamii au majukwaa mengine ya mtandaoni.

Ponografia Isiyoua ya Idhini

Ponografia isiyo ya idhini, pia inajulikana kama "kisasi cha ponografia ya kulipiza kisasi”, ni pale ambapo mtu anashiriki au kutishia kushirikisha picha au video chafu zako bila idhini yako. Hii ni aina kali ya matumizi mabaya ya picha na inaweza kuwa na athari mbaya kwa ustawi wako wa kiakili na kihisia.

Kujiweka Salama wewe mwenyewe

Ikiwa wewe au mtu unayemjua anapitia unayanyasaji wa kutumia picha, hapa chini kuna vidokezo kusaidia kukuweka salama:

  • Tumia Kifaa cha Salama: Ikiwa unaona kuwa kifaa chako kimeathirika, tumia kompyuta au simu ambayo mnyanyasaji hawezi kutumia, kama iliyo kwenye maktaba ya umma.
  • Badilisha Mipangilio ya Faragha: Rekebisha mipangilio ya faragha kwenye akaunti zako za mitandao ya kijamii ili kupunguza ni nani anayeweza kuona maelezo yako.
  • Ripoti na Zuia: Ripoti unyanyasaji kwa jukwaa unapotokea na umzuie mnyanyasaji.
  • Kusanya Ushahidi: Piga picha za skrini za ujumbe wa matusi na machapisho na uyahifadhi kwenye kifaa salama.
  • Tafuta Usaidizi: Zungumza na rafiki au mwanafamilia unayemwamini kuhusu kinachoendelea.

Kukusanya Ushahidi

Ikiwa ni salama, kukusanya ushahidi wa kunyanyaswa kunaweza kusaidia katika upelelezi wa kisheria. Kwa mfano, piga picha za skrini za ujumbe wa matusi na uzihifadhi kwenye kifaa salama. Mtoa huduma wa ukatili wa nyumbani, familia, au kingono, polisi, au mwanasheria anaweza kukushauri kuhusu aina gani ya ushahidi inafaa zaidi kwa kesi yako.

Kupata Msaada

Kabla ya kutafuta msaada, fahamu kuwa hii inaweza kuwa hali hatari kwani unyanyasaji unaweza kuwa mbaya zaidi. Huduma ya unyanyasaji wa nyumbani, familia na kingono inaweza kukusaidia kufanya mpango wa usalama.

eSafety Commissioner imeunda nyenzo katika lugha yako ili kusaidia watu wanaopitia unyanyasaji wa kutumia teknolojia.

WESNET pia ina mfufulizo wa nyenzo (Kiingereza tu) juu ya usalama na ufaragha wa wanawake.