Je, Unyanyasaji wa Kutumia Teknolojia ni nini?
Unyanyasaji wa kutumia teknolojia hutokea wakati mtu anapotumia teknolojia ya kidijitali kumdhibiti, kumlazimisha, au kumdhara mtu mwingine. Mara kwa mara aina hii ya unyanyasaji ni sehemu ya ukatili wa nyumbani, familia, na kingono.
Nchini Australia, baadhi ya aina za unyanyasaji wa kutumia teknolojia, kama vile kushiriki picha za siri bila ruhusa au kutumia programu ya ufuatiliaji ili kumpeleleza mtu, ni kinyume na sheria. Unaweza kuripoti matendo hayo kwa polisi na kwa eSafety Commissioner.
Unyanyasaji wa kutumia teknolojia ni suala kubwa kwa sababu huingilia faragha yako na unaweza kusababisha madhara makubwa. Kuuelewa aina hii ya unyanyasaji ni muhimu ili kujilinda mwenyewe na wengine. Kwa kujua haki zako na kutafuta usaidizi, unaweza kupata udhibiti tena na kuhakikisha usalama wako.
Nchini Australia, ni muhimu kukumbuka:
- Una haki ya kutumia teknolojia bila kuogopa unyanyasaji.
- Unyanyasaji wa kutumia teknolojia kamwe siyo kosa lako.
- Msaada unapatikana, na hauko peke yako.
Aina za Unyanyasaji wa Kutumia Teknolojia
Unyanyasaji wa kutumia teknolojia unaweza kuwa wa aina nyingi. Hapa chini ni mifano:
- Kudhibiti Nenosiri za WiFi: Kukuzuia kutumia mtandao ili kukutenga.
- Kuwasiliana Nawe Kila Mara: Kupiga simu au kutuma ujumbe mara kwa mara ili kujua upo wapi na unachofanya.
- Kufuatilia Shughuli za Mtandaoni: Kuangalia mawasiliano yako ya mtandao wa kijamii, ujumbe wa maandishi, au matumizi ya mtandao.
- Kuzuia Matumizi ya Kifaa: Kukosa kukuruhusu kuwa na simu au kompyuta, au kuongea na marafiki na wanafamilia mtandaoni.
- Kushiriki Picha za Siri Bila Idhini: Kuweka mtandaoni au kutuma picha zako za siri bila ruhusa yako.
- Kumtia Mtu Aibu ya Kitamaduni au Kidini: Kushiriki picha zinazowakilisha vibaya mazoea yako ya kitamaduni au kidini bila idhini yako.
- Kupeleleza na Kufuatilia: Kutumia programu au vifaa ili kufuatilia mahali uliko au shughuli bila ufahamu wako.