Je, Kupuuzwa ni Nini?
Kupuuzwa hutokea ambapo mtu hatoi matunzo na usaidizi unaohitajika kwa ajili ya ustawi wa mtu. Huku kunaweza kujumuisha kukosa kutoa chakula kinachofaa, makao, matibabu, au usaidizi wa kihisia. Kupuuza ni tatizo kubwa na kunaweza kutokea kwa mtu yeyote, lakini ni hatari hasa kwa watu wenye ulemavu.
Kupuuzwa ni tatizo kubwa kwa sababu kunadhuru ustawi wa watu wenye ulemavu. Kuelewa kupuuzwa ni nini na jinsi ya kupata msaada ni muhimu ili kujilinda na wengine. Kwa kujua haki zako na kutafuta msaada, unaweza kuhakikisha usalama na ustawi kwa kila mtu.
Nchini Australia, ni muhimu kukumbuka:
- Una haki ya kutunzwa na kusaidiwa.
- Kupuuzwa kamwe siyo kosa lako.
- Msaada unapatikana, na hauko peke yako.
Ikiwa wewe ni mlezi, ni muhimu kukumbuka kuwa una wajibu kuhakikisha kwamba mtu unayemtunza ana heshima na anasaidiwa vizuri.
Aina za Kupuuzwa
Kupuuzwa huweza kuwa katika aina nyingi. Hapa chini ni baadhi ya mifano:
- Kupuuzwa kwa Kimwili: Kutotoa chakula cha kutosha, nguo safi, au mazingira salama ya kuishi.
- Kupuuzwa kwa Kimatibabu: Kutompa dawa zilizohitajika, matibabu, au miadi ya matibabu.
- Kupuuzwa kwa Kihisia: Kutompa usaidizi wa kihisia, upendo au uangalizi.
- Kupuuzwa kwa Kielimu: Kutotoa fursa au usaidizi unaohitjika wa kielimu.
Mtu yeyote anaweza kuathirika na kupuuza, lakini watu wenye ulemavu wako hatarini hasa. Huu unaweza kujumuisha watoto, watu wazima, na wazee wenye ulemavu wa kimwili au kiakili.