Watu wenye ulemavu wanakabiliwa na viwango vya juu vya unyanyasaji na vurugu. Wanawake wenye ulemavu wana uwezekano mkubwa wa kupitia ukatili wa kijinsia na unyanyasaji kutoka kwa wapenzi wa karibu.
Wanawake wenye ulemavu wanaweza kukabiliwa na aina tofauti za unyanyasaji na ukatili, kama wanawake wengine. Hata hivyo, wao pia hukabiliiwa na matatizo ya kipekee yanayoweza kufanya iwe ni vigumu kwao kupata msaada.
Hapa chini ni baadhi ya mifano:
- Unyanyasaji wa Kimwili: Huu unaweza kujumuisha vitendo vinavyosababisha madhara ya kimwili au maumivu. Mifano ni kama kupiga, kupiga kofi, au kusukuma. Inajumuisha pia kutotoa dawa zinazohitajika, kuondoa huduma za usaidizi, au kumzuia mtu kimwili.
- Ukatili wa Kingono: Huu unaweza kuhusisha kulazimishwa kufanya matendo ya ngono kwa malipo ya huduma au usaidizi.
- Unyanyasaji wa Kihisia: Huu unajumuisha kutishiwa kupelekwa kwenye kituo cha matunzo bila mapenzi yao au kuzuiwa kuonana na wanafamilia na marafiki.
- Unyanyasaji wa Kichumi: Huu unahusisha kuiba pesa au malipo ya ulemavu.
- Udhibiti wa Kulazimisha: Huu ni pale ambapo mtu anamdanganya mtu mwingine afikirie kuwa unyanyasaji ni jambo la kawaida katika mahusiano yote.
- Unyanyasaji wa Uzazi: Huu unaweza kuhusisha kulazimishwa kupata utaratibu wa kimatibabu kama vile kufunga kizazi bila idhini. Kufunga uzazi kunamaanisha kufanya mtu asiweze kupata watoto.
Kupata Msaada
Women with Disabilities Australia imeunda nyenzo ya bure yenye maelezo ya ukatili, unyanyasaji, na usalama. Nyenzo hii iliundwa kwa usaidizi wa wanawake, wasichana, na watu wa jinsia tofauti wenye ulemavu.
Ikiwa wewe au mtu unayemjua amepitia unyanyasaji, kumbuka siyo kosa lako. Hakuna kinachohalalisha vurugu hii. Msaada unapatikana.
1800RESPECT: Piga simu kwa 1800 737 732 kupata msaada na ushauri wa siri.
Huduma za Msaada wa Kisheria: Hutoa ushauri na msaada wa kisheria bila malipo. Wanaweza kueleza haki zako na kukasaidia na masuala ya kisheria. Unaweza kuwasiliana na msaada wa kishiera katika jimbo lako au wilaya yako hapa.
Kupata habari na usaidizi zaidi, tembelea Ukurasa wetu wa Huduma za Usaidizi.