Usawa wa kijinsia unamaanisha kuwa kila mtu nchini Australia – bila kujali jinsia yake - ana haki na majukumu sawa. Kila mtu anapaswa kuweza kuishi maisha yake bila vurugu na kupata fursa sawa.
Usawa wa kijinsia huathiri kila mtu, ikijumuisha wanaume, wanawake, wavulana, wasichana, na watu wa jinsia tofauti. Kufikia usawa mzima wa jinsia nchini Australia kungekuwa na faida nyingi kwa kila mtu, kama vile kuzuia ukatili wa kijinsia, kuboresha uchumi wetu au kuwa na jumuiya za imara na afya zaidi.
Hata hivyo, kuna tofauti za usawa na itikadi wa kijinsia inayotuzuia kufikia usawa wa kijinsia nchini Australia. Kwa mfano, wanawake wanatumia muda mrefu zaidi bado kufanya ulezi bila kulipwa, kupata kipato kidogo, kupitia viwango juu ya ukatili wa kijinsia na wanakabiliwa na vikwazo zaidi vya kuwepo katika majukumu ya uongozi.
Watu wenye jinsia tofauti hawawezi kuonyesha jinsia yao nje ya mfumo wa jadi wa jozi wa jinsia na wanapitia ubaguzi, unyanyapaa na kutengwa.
Wanaume na wavulana wanapitia itikadi mbaya ambazo zinaathiri afya yao ya kimwili na kihisia. Itikadi ngumu za uanaume huweka shinikizo kwa wanaume kuwa na tabia fulani kama vile kuwa mgumu, kutawala na kuacha kuonyesha hisia zao.
Kufikia usawa wa kijinsia nchini Australia ni wajibu wa kila mtu na utanufaisha kila mtu katika jumuiya.
Serikali ya Australia imetoa Working for Women: A Strategy for Gender Equality ambayo inaeleza ni nini kinachohitajika ili kuwa na Australia yenye usawa wa kijinsia.