Unyanyasaji wa Kiroho

Je, Unyanyasaji wa Kiroho ni nini?

Unyanyasaji wa kiroho ni pale ambapo mtu anatumia imani yako ya kidini au ya kiroho kukuumiza, kukutishia, au kukutawala. Huu unaweza kutokea pamoja na aina nyingine za unyanyasaji na ukatili wa nyumbani na familia.

Mtu yeyote anaweza kupitia unyanyasaji wa kiroho, bila kujali imani zake za kidini au za kiroho. Asili, dini, au imani yako sio sababu ya unyanyasaji huo.

Je, Unyanyasaji wa Kiroho Unaweza Kutokea Wapi?

Unyanyasaji wa kiroho unaweza kutokea katika vikundi vya kidini ili kudhibiti washiriki au katika uhusiano wa wenzi wa karibu.

Mifano ya Unyanyasaji wa Kiroho

  • Kutokuruhusu kufuata dini yako kabisa au vile kama ungependa kufuata.
  • Kukulazimisha kushiriki katika mazoea ya kidini ambayo hutaki kushiriki.
  • Kutumia vibaya viongozi wa kidini au mafundisho ya kidini kukulazimisha kubaki kwenye uhusiano au kuhalalisha vurugu na unyanyasaji.
  • Kukuaibisha au kukutukana kwa imani yako ya kidini ili kukuumiza.

Kutambua Unyanyasaji wa Kiroho

Unyanyasaji wa kiroho unaweza kuwa vigumu kutambua, lakini hudhuru sawa na aina zingine za unyanyasaji. Hapa chini ni baadhi ya ishara :

  • Kuhisi kushinikizwa kufuata mazoea ya kidini ambayo hukubaliani nayo.
  • Kutengwa na jumuiya yako ya kidini.
  • Kuhisi hatia au hofu kwa sababu ya imani yako ya kidini kutokana na matendo ya mtu fulani.
  • Kuambiwa kwamba kuacha uhusiano wa kunyanyasa ni kinyume na dini yako.

Kupata Msaada

Kumbuka, hauko peke yako, na msaada unapatikana.

Ikiwa wewe au mtu unayemjua amepitia unyanyasaji wa kiroho, msaada unapatikana.

Ikiwa unahitaji usaidizi na sio dharura, tembelea Ukurasa wetu wa Huduma za Usaidizi. Wanaweza kutoa msaada na mwongozo.

Kumbuka:

  • Una haki ya kufuata dini yako kwa uhuru.
  • Hakuna mtu anayepaswa kutumia imani yako kudhibiti au kukudhuru,
  • Usaidizi unapatikana, na hauko peke yako.