Unyanyasaji wa Kijamii

Je, Unyanyasaji wa Kijamii ni nini?

Unyanyasaji wa kijamii hutokea mtu anapodhibiti miingiliano yako ya kijamii na mahusiano yako. Huu unaweza kujumuisha kukutengwa na marafiki, wanafamilia na shughuli za jumuiya. Unyanyasaji wa kijamii ni aina ya ukatili wa nyumbani na familia na unaweza kufanya uhisi peke yako na kutegemea mnyanyasaji yule.

Unyanyasaji wa kijamii ni tatizo kubwa kwa sababu unakutenga na kufanya uhisi peke yako. Ni muhimu kuelewa unyanyasaji wa kijamii ni nini na jinsi ya kupata msaada. Kwa kujua haki zako na kutafuta usaidizi, unaweza kuungana tena na watu na kuanza kujenga tena maisha yako ya kijamii.

Nchini Australia:

  • Una haki kuwa na mahusiano na miingiliano ya kijamii bila kudhibitiwa.
  • Unyanyasaji wa kijamii kamwe siyo kosa lako.
  • Msaada unapatikana, na hauko peke yako.

Aina za Unyanyasaji wa Kijamii

Unyanyasaji wa kijamii unaweza kutokea kwa aina nyingi, kama vile:

  • Kutengwa: Kukuweka mbali na marafiki, wanafamilia, na shughuli za kijamii.
  • Kufuatilia: Kuangalia mara kwa mara mahali unapoenda, unaongea na nani, na unachofanya.
  • Kudhibiti Mawasiliano: Kukuzuia usitumie simu, mtandaoni, au njia nyingine za kuwasilana na wengine.
  • Udhalilishaji Hadharani: Kukutukana au kukuaibisha mbele ya wengine ili kuharibu mahusiano yako.
  • Wivu na Kuonyesha Kukumiliki: Kuonyesha wivu na kukumiliki ili kukuzuia kuwa na mahusiano mengine.

Mtu yeyote anaweza kuwa mwaathirika wa unyanyasaji wa kijamii, bila kujali umri, jinsia, au asili. Wanawake wahamiaji na wakimbizi huenda wanakabiliana changamoto za ziada kutafuta msaada, kama vikwazo vya lugha na ukosefu wa mitandao ya usaidizi.

Kutambua Unyanyasaji wa Kijamii

Kutambua na kushughulikia unyanyasaji wa kijamii kunaweza kuwa vigumu, lakini ishara zinajumuisha:

  • Kuhisi kutengwa na marafiki na wanafamilia.
  • Kufuatiliwa au kufuatwa na mwenzi wako au mwanafamilia.
  • Mawasiliano yako yanazuiwa au kudhibitiwa.
  • Kuhisi kudhalilishwa au kuaibishwa haradharani.
  • Kupitia wivu au kumilikiwa na mwenzi wako au mwanafamilia.

Athari ya Unyanyasaji wa Kijamii

Unyanyasaji wa kijamii huweza kusababisha madhara yote ya haraka na ya muda mrefu:

  • Maumivu ya Kihisia: Hisia za upweke, huzuni, au unyogovu.
  • Kupoteza Usaidizi: Kupoteza mawasiliano na marafiki na wanafamilia ambao wanaweza kutoa usaidizi na kuunga mkono nawe.
  • Utegemezi: Kujisikia kutegemea mnyanyasaji kwa mwingiliano wa kijamii na usaidizi.
  • Kujithamini Chini: Kujiona aibu au huna thamani kwa sababu ya unyanyasaji.

Kupata Msaada

Ikiwa unapitia unyanyasaji wa kijamii, ni muhimu kutafuta msaada. Kuna nyenzo na huduma zinazopatikana kukusaidia.

1800RESPECT: Piga simu kwa 1800 737 732 kupata usaidizi na huduma ya siri.

Australian Federal Police: Piga simu kwa 131 237 au temblea tovuti yao.

Huduma za Msaada wa Kisheria: Hutoa ushauri na msaada wa bure wa kisheria. Wanaweza kueleza haki zako na kukusaidia na masuala ya kisheria. Unaweza kuwasiliana na msaada wa kisheria katika jimbo lako au wilaya yako hapa.

Huduma za Jamii: Mashirikia mengi ya mahali yanasaidia wanawake wahamiaji na wakimbizi kupata msaada.

Huduma za Ushauri Nasaha: Washauri wa kitaalamu wanaweza kutoa usaidizi wa kihisia na ushauri wa vitendo.

Kupata habari na usaidizi zaidi, tembelea Ukurasa wetu wa Huduma za Msaada.