Unyanyasaji wa Kisaikolojia

Je, Unyanyasaji wa Kisaikolojia ni Nini?

Unyanyasaji wa kisaikolojia hutokea mtu anapotumia maneno na matendo kukudhibiti, kukuogopesha, au kukudhuru kwa kihisia. Aina hii ya unyanyasaji inaweza kufanya uhisi bila thamani, kuogopa, au kutengwa. Unyanyasaji wa kisaikolojia unaweza kutokea katika uhusiano wowote, ukijumuisha wanafamilia, wenzi, au walezi.

Unyanyasaji wa kisaikolojia ni tatizo kubwa kwa sababu unasababisha madhara ya kihisia. Ni muhimu kuelewa unyanyasaji wa kisaikolojia ni nini na jinsi ya kupata msaada. Kwa kujua haki zako na kutafuta usaidizi, unaweza kujilinda mwenyewe, na kuanza kuponya.

Nchini Australia ni kinyume na sheria kunyanyasa mtu:

  • Una haki ya kuishi bila kuumizwa kwa kihisia wala kudhibitiwa.
  • Unyanyasaji wa kisaikolojia kamwe siyo kosa lako.
  • Msaada unapatikana, na hauko peke yako.

Aina za Unyanyasaji wa Kisaikolojia

Unyanyasaji wa kisaikolojia unaweza kutokea kwa aina nyingi, kama vile:

  • Vitisho: Kusema atakudhuru wewe, watoto wako, au wanyama wako.
  • Udhalilishaji: Kukutukana, kukuita majina, au kufanya ujisikie vibaya juu yako.
  • Kutengwa: Kukuweka mbali na marafiki, wanafamilia, na wasaidizi wengine.
  • Udhibiti: Kukuambia nini cha kufanya, nini cha kuvaa, au mahali unaporuhusiwa kwenda.
  • Kisingizio (Gaslighting): Kukufanya uwe na mashaka juu ya mawazo yako na hisia zako kwa kukataa ukweli au kukulaumu kwa mambo ambayo siyo kosa lako.

Mtu yeyote anaweza kuwa mwaathirika wa unyanyasaji wa kisaikolojia, bila kujali umri, jinsia, au asili. Wanawake wahamiaji na wakimbizi huenda wanakabiliana changamoto za ziada kutafuta msaada, kama vikwazo vya lugha na ukosefu wa mitandao ya usaidizi.

Kutambua Unyanyasaji wa Kisaikolojia

Kutambua na kushughulikia unyanyasaji wa kisaikolojia kunaweza kuwa vigumu, lakini ishara zinajumuisha:

  • Kujisikia Huna Thamani: Daima kujisikia vibaya juu yako mwenyewe au kukutilia shaka kujithamini mwenyewe.
  • Hofu: Kuogopa mwenzi au mwanafamilia wako na anachoweza kufanya.
  • Kutengwa: Kuwekwa mbali na marafiki, wanafamilia, na watu wengine wanaokujali.
  • Kuchanganyikiwa: Kujitilia shaka mawazo yako yenyewe na hisia kwa sababu ya mnyanyasaji anachosema.
  • Utegemezi: Kuhisi kama huwezi kufanya maamuzi au kufanya mambo bila ruhusa ya mnyanyasaji.

Athari ya Unyanyasaji wa Kisaikolojia

Unyanyasaji wa kisaikolojia huweza kusababisha madhara yote ya haraka na ya muda mrefu:

  • Maumivu ya Kihisia: Hisia za hofu, wasiwasi, au unyogovu.
  • Masuala ya Afya ya Kiakili: Masuala ya muda mrefu kama ugonjwa wa mkazo wa baada ya mateso (PTSD).
  • Kupoteza Kujiamini: Ugumu wa kuamini maamuzi na hisia zako.
  • Kutengwa kwa Kijamii: Kupoteza mawasiliano na marafiki na wanafamilia.

Kupata Msaada

Ikiwa unapitia unyanyasaji wa kisaikolojia, ni muhimu kutafuta msaada. Kuna nyenzo na huduma zinazopatikana kukusaidia.

1800RESPECT: Piga simu kwa 1800 737 732 kupata usaidizi na huduma ya siri.

Australian Federal Police: Piga simu kwa 131 237 au tembelea tovuti yao.

Huduma za Msaada wa Kisheria: Hutoa ushauri na msaada wa bure wa kisheria. Wanaweza kueleza haki zako na kukusaidia na masuala ya kisheria. Unaweza kuwasiliana na msaada wa kisheria katika jimbo lako au wilaya yako hapa.

Kupata habari na usaidizi zaidi, tembelea Ukurasa wetu wa Huduma za Msaada.