Unyanyasaji wa Mahari

Je, Mahari ni nini?

Mahari ni desturi ya jadi ambapo fedha, mali, au zawadi hutolewa kutoka kwa familia moja hadi familia nyingine karibia wakati wa ndoa. Desturi hii ni halali nchini Australia.

Maozea Mbalimbali ya Kitamaduni

  • Katika jumuiya za Asia Kusini, mara nyingi familia ya bibi-arusi huwapa familia ya bwana harusi pesa, vito, mali, magari, na vifaa vya nyumbani.
  • Katika jumuiya za Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati, familia ya bwana harusi inaweza kutoa pesa au ng’ombe kwa familia ya bibi-arusi.
Je, Unyanyasaji wa Mahari ni Nini?

Je, Unyanyasaji wa Mahari ni Nini?

Unyanyasaji wa mahari hutokea ambapo mtu anatumia desturi ya mahari ili kuumiza, kudhibiti, au kudai zaidi kutoka kwa mtu mwingine. Unyanyasaji huu unakuwa tatizo kubwa nchini Australia, hasa kwa wanawake wenye viza za muda wanaotegemea wapenzi wao kwa ukazi. Huenda wanaweza kutishiwa kwamba watapoteza   viza zao ikiwa hawatatoa mahari zaidi.

Aina za Unyanyasaji wa Mahari

Aina za Unyanyasaji wa Mahari

Unyanyasaji wa mahari ni aina ya unyanyasaji wa nyumbani na familia. Inaweza kutokea pamoja na matumizi mabaya mengine kama vile unyanyasaji wa kifedha, wa kimwili au kihisia.

Dalili za Unyanyasaji wa Mahari

Dalili za Unyanyasaji wa Mahari

Inaweza kuwa vigumu kuona kama unyanyasaji wa mahari unatokea kwako au kwa mtu unayemjua. Hapa chini kuna baadhi ya ishara:

  • Mume anajaribu kudhibiti mapato ya mke wake, akaunti za benki, na simu yake.
  • Familia ya bibi harusi kulazimika kutoa zawadi ili kuepuka aibu katika jamii yao.
  • Mume anatishia vurugu ikiwa mke wake hatakidhi matakwa yake ya mahari au ya familia yake.
  • Wanandoa hawawezi kufanya maamuzi yao wenyewe kutokana na mienendo isiyo ya haki ya nguvu za familia.

Kupata Msaada

Ikiwa wewe au mtu unayemjua anapitia unyanyasaji wa mahari, ni muhimu kupata msaada. Hapa chini ni hatua unazoweza kuchukua:

  • Zungumza na Mtu Unayemwamini: Shirikisha kinachotokea na rafiki, mwanafamilia, au mtu fulani katika jumuiya yako unayemwamini.
  • Tafuta Usaidizi wa Kitaalamu: Wasiliana na mtoa huduma ya ukatili wa nyumbani, familia, na kingono. Anaweza kutoa usaidizi na mwongozo juu ya kufanya nini baadaye.
  • Jua Haki Zako: Kuelewa haki zako za kisheria kunaweza kukusaidia kufanya maamuzi sahihi. Kuna sheria zinazokulinda dhidi ya unyanyasaji.
  • Tumia Nyenzo Zinazopatikana: Harmony Alliance na Australasian Centre for Human Rights and Health zina nyenzo katika lugha yako kuhusu unyanyasaji wa mahari nchini Australia. Hizi zinaweza kutoa maelezo na usaidizi zaidi.

Huduma za Msaada

Ikiwa unahitaji usaidizi na suala hilo siyo la  dharura, watoa huduma wa unyanyasaji wa nyumbani, familia na kingono wanaweza kukusaidia. Tembelea [Ukurasa wa Huduma za Usaidizi] wetu kupata habari zaidi. Wanaweza kusaidia na:

  • Ushauri wa kisheria
  • Ushauri nasaha
  • Malazi salama
  • Usaidizi wa kipesa

Kumbuka, hauko peke yako, na msaada unapatikana.

Ikiwa wewe au mtu unayemjua amepitia unyanyasaji wa mahari, kumbuka siyo kosa lako. Hakuna kinachohalalisha vurugu hii. Msaada unapatikana.

1800RESPECT: Piga simu kwa 1800 737 732 kupata msaada na ushauri wa siri.

Huduma za Msaada wa Kisheria: Hutoa ushauri na msaada wa kisheria bila malipo. Wanaweza kueleza haki zako na kukasaidia na masuala ya kisheria. Unaweza kuwasiliana na msaada wa kishiera katika jimbo lako au wilaya yako hapa.

Kupata habari na usaidizi zaidi, tembelea Ukurasa wetu wa Huduma za Usaidizi.