Utumwa wa Nyumbani

Je, Utumwa wa Nyumbani ni nini?

Utumwa wa nyumbani ni aina ya utumwa wa kisasa. Unatokea pale ambapo mtu analazimishwa kufanya kazi nyumbani na hawezi kuondoka. Anadhibitiwa na vitisho au uongo na hana uhuru. Nchini Australia, hili ni kosa kubwa la jinai..

Nchini Australia:

  • Una haki za uhuru na hali za kazi ya haki.
  • Hakuna mtu anayepaswa kukulazimisha kufanya kazi kinyume na mapenzi yako.
  • Msaada unapatikana, na hauko peke yako.

Je, Nani Anaweza Kuathirika?

Mtu yeyote anaweza kuwa mwathirika wa utumwa wa nyumbani, lakini waathirika wengi ni wanawake na wasichana. Unaweza kutokea kwa watu kutoka asili yoyote, ikiwa ni pamoja na wanaume na wavulana.

Utumwa wa nyumbani unaweza kuonekana kama kazi ya kawaida ya nyumbani (kama kusafisha au kupika), lakini ni unyonyaji. Ina maana mtu anatendewa na unyanyasaji na bila haki.

Waathirika mara kwa mara:

  • Hudanganywa Kuhusu Hali za Kazi: Wanadanganywa kuhusu kazi itakuwaje.
  • Hutengwa: Wanawekwa mbali na marafiki, familia, na jamii.
  • Hutishiwa au Kuumizwa: Wanakabiliwa na vitisho au vurugu halisi.
  • Hulipwa Kidogo au Kutolipwa Kabisa: Wanapata pesa kidogo au kutolipwa pesa kwa kazi yao.
  • Hawana Udhibiti wa Hati za Vitambulisho: Hawana ufikiaji wa pasipoti yao au hati nyingine zao za vitambulisho.
  • Kufungwa na Deni: Wanadai pesa kwa usafiri au viza na hawawezi kondoka hadi irudishwa. Wakati mwingine wanafamilia ambapo wapo n’gambo wanatishiwa kama deni halijalipwa.

Dalili za Utumwa wa Nyumbani

  • Kulazimishwa kufanya kazi masaa mengi kwa malipo kidogo au kutolipwa chochote.
  • Kutoruhusiwa kuondoka mahali pa kazi.
  • Kutengwa mbali na marafiki, familia, au jamii
  • Kukabiliwa na vitisho au vurugu halisi.
  • Kutokuwa na udhibiti wa hati za utambulisho wa kibinafsi kama pasipoti.
  • Kuwa na deni la kusafiri au viza.

Kupata Msaada

Ikiwa wewe au mtu unayemjua anapitia utumwa wa nyumbani, msaada unapatikana.

Australian Red Cross Support for Trafficked People Program: Piga simu kwa 03 9345 1800 au tuma barua pepe kwa national_STPP@redcross.org.au

Australian Federal Police: 131 237 au nenda kwenye tovuti ya AFP.

The Australian Red Cross imeunda nyenzo katika lugha yako ambazo zinaweza kukusaidia kuelewa utumwa wa kisasa.