Ukatili wa Nyumbani na wa Familia

Je, Ukatili wa Nyumbani na Familia ni nini?

Ukatili wa nyumbani na familia ni ukatili wowote unaotokea kati ya wanafamilia. Huu unaweza kujumuisha vurugu kati ya wapenzi wa sasa au wa zamani, wanandoa, mzazi na mtoto, au wanandugu. Wakati mwingine huitwa unyanyasaji wa wenzi.

Ukatili wa nyumbani na familia ni tatizo kubwa kwa sababu unasababisha madhara na hofu. Kuuelewa ni muhimu ili kujilinda mwenyewe na wengine. Kwa kujua haki zako na kutafuta usaidizi, unaweza kusaidia kukomesha vurugu hii na kuhakikisha usalama kwa kila mtu.

Nchini Australia ukatili wa nyumbani na wa familia ni kinyume cha sheria:

  • Una haki ya kuishi bila woga wala unyanyasaji.
  • Ukatili wa nyumbani na familia kamwe siyo kosa lako.
  • Msaada unapatikana, na hauko peke yako.

Ukatili wa nyumbani na familia ni muundo unaorudiwa wa tabia unaotumiwa kumdhibiti mtu mwingine katika familia au uhusiano wa karibu. Humfanya mwathirika ahisi hofu kwa usalama wake au usalama wa watu wengine.

Kutumia vurugu, vitisho, au kumdhibiti mtu ni uchaguo. Kuchagua ukatili sio sawa kamwe. Kuna msaada unaopatikana ili kukomesha kutumia ukatili.

Je, ni Nani Anaweza Kuathiriwa?

Ukatili wa nyumbani na familia unaweza kutokea katika aina yoyote ya ushusiano, sio tu kati ya wapenzi au wanandoa. Unaweza kutokea katika:

  • Mahusiano ya karibu kati ya watu wa jinsia yoyote
  • Mahusiano ya mzazi au mzazi wa kambo kwa mtoto
  • Watunzaji wananyanyasa watu wenye ulemavu
  • Watoto wanaonyanyasa wazazi wao au wanafamilia wengine
  • Mahusiano ya jamaa
  • Wanafamilia wa jamaa

Aina za Ukatili wa Nyumbani na Familia

Ukatili wa nyumbani na familia una aina nyingi. Mara kwa mara, waathirika hupata zaidi kuliko aina moja ya unyanyasaji kwa wakati mmoja. Aina za unyanyasaji zinajumuisha:

  • Unyanyasaji wa kutumia teknolojia
  • Udhibiti wa kulazimisha
  • Unyanyasaji wa kifedha
  • Ukatili wa kingono
  • Ukatili wa kisaikolojia
  • Unyanyasaji wa kijamii
  • Unyanyasaji wa mahari
  • Unyanyasaji wa kiroho
  • Utumwa wa ndani
  • Unyanyasaji wa wazee
  • Unyanyasaji wa watoto
  • Unyanyasaji wa kimwili
  • Ukeketaji na kukatwa kwa wanawake

Kutambua Ukatili wa Nyumbani na Familia

Ikiwa wewe au mtu unayefahamu anapitia vurugu, inaweza kuwa vigumu na wakati mwingine sio salama kuizungumzia. Watu wengine huenda hata wasitambue kuwa wanapitia vurugu.

Ikiwa ni salama, unaweza kumwuliza kuhusu hali yake na kumjulishe kuwa una wasiwasi naye na kwamba unataka kumsaidia. Ikiwa hayuko tayari kuzungumza, mjulishe utakuwepo kwa ajili yake wakati atakapokuwa tayari kuongea.

Kupata Msaada

Ikiwa wewe au mtu unayemfahamu yupo katika hatari ya haraka, piga simu kwa triple zero ‘000’.

Ikiwa unahitaji msaada ambao sio ya haraka, mtoa huduma wa ukatili wa nyumbani, familia na kingono anaweza kukusaidia. Tembelea Ukurasa wetu wa Huduma za Usaidizi.

1800RESPECT: Piga simu kwa 1800 737 732 kwa msaada na ushauri wa siri.

Unaweza kuwasiliana na Support for Trafficked People Program kwa 03 9345 1800 au kwa national_STPP@redcross.org.au

Unaweza kuwasiliana na Australian Federal Police kwa 131 237 au enda kwa tovuti ya AFP.

Huduma za Msaada wa Kisheria: Hutoa ushauri wa kisheria na msaada. Wanaweza kueleza haki zako na kukusaidia na masuala ya kisheria. Unaweza kuwasiliana na msaada wa kisheria katika jimbo lako au wilaya yako kwa hapa.