Women’s Safety Hub ilibuniwa kwa usaidizi wa wanawake wahamiaji na wakimbizi. Inatoa maelezo katika lugha tofauti kwa wale walio katika hatari ya au kukumbana na ukatili wa nyumbani, wa familia na kingono. Nyenzo hizi husaidia wanawake kupata taarifa na usaidizi wanaohitaji.
Nyenzo hii ni sehemu ya mjadala mkubwa kuhusu ukatili wa kijinsia na usalama wa wanawake. Inaangazia mahitaji maalum ya wanawake wahamiaji na wakimbizi nchini Australia. Pia inasisitiza katika kuonyesha umuhimu wa huduma usalama za kitamaduni kwa masuala nyeti, mahusiano ya heshima na kuboresha jinsi tunavyosaidia jamii mbalimbali za Australia.
Harmony Alliance iliunda Women’s Safety Hub. Nyenzo hii imebuniwa kwa wanawake wahamiaji na wakimbizi, ikitoa taarifa inayoakisi uzoefu wao na mahitaji yao nchini Australia. Kitovu hiki kinalenga kusaidia usalama na ustawi wao.
Unaweza kujifunza zaidi kuhusu Harmony Alliance: Migrant and Refugee Women for Change kwenye tovuti yetu.
Tunawashukuru wajumbe wa Harmony Alliance, wanajamii, na wataalamu wa usalama wa wanawake ambao walisaidia kuunda nyenzo hii. Pia tunatambua na kuthamini ushirikiano na juhudi za Australasian Centre for Human Rights and Health kwa usaidizi wao katika wakati wote wa mradi na kwa ujuzi wao wa pamoja na utaalamu juu ya unyanyasaji wa mahari nchini Australia.