Women’s Safety Hub

Women’s Safety Hub ni nyenzo ya lugha za tamaduni mbalimbali  iliyobuniwa na michango wa wanawake wahamiaji na wakimbizi, mashirika ya kijamii, na watoa huduma wenye utaalamu kupitia mchakato wa kubuni pamoja.

Soma zaidi

Kuhusu Women’s Safety Hub

Wanawake wahamiaji na wenye asili ya ukimbizi wanaweza kutumia Women’s Safey Hub kupata taarifa katika lugha yao yenyewe inayofaa kwa mahitaji yao. Kitovu hiki kinashughulikia mada nyingi kama vile ukatili wa nyumbani na familia, ukatili wa kingono, udhibiti wa kulazimisha na unyanyasaji wa kifedha. Pia kinatoa mwongozo kuhusu unyanyasaji unaotumia teknolojia, unyanyasaji wa kisaikolojia na unyanyasaji wa kijamii. Zaidi ya hayo, Women’s Safey Hub kinatoa maelezo ya huduma maalum na watoa huduma wengine za usaidizi wanaosaidia wanawake wahamiaji na wakimbizi. Nyenzo hii hulenga kusaidia usalama na ustawi wa wanawake, kuhakikisha wanapata usaidizi na taarifa wanazohitaji.

Kuhusu Harmony Alliance

Kuhusu Harmony Alliance

Harmony Alliance: Migrant and Refugee Women for Change ni mojawapo ya Miungano sita ya Kitaifa ya Wanawake nchini Australia. Inaungwa mkono na Serikali ya Australia. Lengo lake ni kuhakikisha kuwa wanawake wote nchini Australia wanaweza kushiriki maoni yao na sauti zao zisikike katika maamuzi yanayowahusu. 

Soma zaidi
Ukatili wa Kijinsia

Ukatili wa Kijinsia

Ukatili wa kijinsia ni ukatili wowote unaoelekezwa kwa mtu kwa sababu ya jinsia yake. Aina hii ya ukatili huathiri zaidi wanawake na wasichana, lakini inaweza kuathiri mtu yeyote. Huitwa pia ukatili dhidi ya wanawake.

Soma zaidi
Huduma Za Usaidizi

Huduma Za Usaidizi

Tafuta huduma za usaidizi kulingana na eneo na kategoria.

Soma zaidi

Ikiwa wewe au mtu unayemfahamu yupo katika hatari ya haraka, piga simu kwa triple zero ‘000’.

Ikiwa unahitaji msaada ambao sio ya haraka, mtoa huduma wa ukatili wa nyumbani, familia na kingono anaweza kukusaidia. Tembelea Ukurasa wetu wa Huduma za Usaidizi.

Shiriki maoni yako nasi

Fikisha